Ligi Ya Wanawake

Simba Queens kuwafuta machozi Simba

KLABU ya Simba Queens inahitaji pointi tatu kupata uhakika wa kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara kwa msimu wa 2023/24.

Simba Queens inaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 43 baada ya michezo 15.

Akizungumza na Spotileo, Kocha Mkuu wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi, amesema malengo ni kuona timu yake inatwaa taji hilo bila ya kupoteza mechi.

“Hatuangalii mechi tunahitaji kushinda kila mechi bila ya kujali tunakutana na timu ipi. Ligi haijaisha, tusipokuwa makini tunaweza kupoteza malengo,”amesema kocha huyo.

Mgosi amesema watahakikisha wanafanya vizuri katika michezo mitatu iliyosalia ili kurejesha heshima ya klabu na kuwapa furaha mashabiki wa Simba baada ya timu ya wanaume kutofanya vizuri.

Simba Queens imebakiza mechi dhidi ya Fountain Gate Princess Juni 10 na Geita Gold Queens Juni 14 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam huku wakicheza ugegeni Juni 7 dhidi ya Alliance Girls.

Related Articles

Back to top button