FANyumbani

Raundi ya 2 ASFC kutimua vumbi leo

RAUNDI ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) inaanza leo kwa michezo minne viwanja tofauti.

Kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wenyeji Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Greenland.

Rospa itakuwa mgeni wa Ihefu kwenye uwanja wa Highland Estates uliopo Mbarali, Mbeya.

JKT Tanzania itaikaribisha Kurugenzi kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma utashuhudia Magereza ikipambana na wenyeji Dodoma Jiji.

Related Articles

Back to top button