KwinginekoSerie A
Pogba afungiwa miaka 4
KIUNGO wa Juventus Paul Pogba amefungiwa kucheza mpira wa miguu kwa miaka minne kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United awali alisimamishwa Septemba 2023 baada ya vipimo vya madawa kuonesha ongezeko la homoni kwenye mfumo wa mwili.
Ripoti zimesema huenda Pogba akakata rufani dhidi ya uamuzi huo wa mahakama ya kupambana na madawa ya kuongeza nguvu ya Italia.
Kwa uamuzi huo ina maana Pogba hatacheza hadi 2027 atakapokuwa na umri wa miaka 33.
Juventus ilimsajili tena Pogba kwa mkataba wa miaka minne Julai 2022 baada ya kumaliza mkataba wake Manchester United.
Pogba amecheza jumla ya dakika 51 msimu huu akitokea benchi katika michezo ya Ligi Kuu Italia dhidi ya Bologna na Empoli.