Burudani
Omondi autaka ubunge 2027
KENYA: Mchekeshaji maarufu na mwanaharakati wa kijamii, Eric Omondi ana nia ya kujitosa kwenye Siasa za Kenya, baada ya kudokeza kuwa, huenda akagombea Kiti cha Ubunge wa jimbo la Lang’ata katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027. Akidai hii, “Ni Sauti ya Mungu”.
–
Omondi ameeleza kuwa, nia hiyo imekuja baada uungwaji mkono mkubwa, kutokana na shughuli zake za kijamii anazoziendesha na umaarufu wake ulisababisha wakazi wa Lang’ata kumkaribisha Jimboni.
–
Omondi atakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa mtangazaji wa zamani na Mbunge wa sasa wa Jimbo hilo,Phelix Odiwour maarufu Jalang’o.