Novatus atambulishwa rasmi Shakhtar Donetsk

BEKI wa kimataifa wa Tanzania Novatus Miroshi leo ametambulishwa kujiunga rasmi na klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Novatus mwenye umri wa miaka 20 amehamia Shakhtar kwa mkopo kutoka Zulte Waregem ya Ubelgiji kwa mkataba utakaofikia mwisho msimu wa 2023/24.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Shakhtar Donetsk imeandika: “🧡 Karibu! 🆕 Novatus MiroÅ¡i 🙌🇹🇿 Mtanzania wa kwanza katika historia ya “Shakhtar” âš’.”
Miroshi alianza kucheza Azam na kisha kuhamia Maccabi Tel Aviv ya Israel mwaka 2020.
Aliitumikia Beitar Tel Aviv pia ya Israel msimu wa 2021/22 akicheza mechi 26 na kufunga bao moja.
Katika msimu wa 2022 Novatus alisaini mkataba wa miaka mitatu kukiwasha katika klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji ambapo alicheza mechi 38 na kutoa pasi mbili za mabao.
Shakhtar Donetsk iko kundi H katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na Barcelona ya Hispania, Porto ya Ureno na Antwerp ya Ubelgiji.