Kwingineko

Xavi-Ni huzuni, Dembele anaondoka

MSHAMBULIAJI wa Barcelona Ousmane Dembele atajiunga na Paris Saint-Germain, amesema Kocha Xavi Hernández.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 alikuwa benchi wakati wa mchezo wa kirafiki Barcelona ilipoifunga AC Milan goli 1-0 jijini Las Vegas, Marekani.

“Inaniuma kwa sababu nadhani tumemtunza vizuri hapa ili awe na furaha, aridhike na aendelee kuleta matokeo kwa ajili yetu,” amesema Xavi.

Dembele amefunga magoli 40 katika michezo 185 tangu ajiunge na Barcelona mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya pauni milioni 135 sawa na shilingi bilioni 411.6.

Alisaini mkataba mpya wa miaka miwili Barcelona mwaka uliopita baada ya msimu bora kwake akiwa mchezaji aliyetoa pasi nyingi zaidi za magoli La Liga.

Dembele alifunga goli moja katika ushindi wa magoli 3-0 wa ‘El Clásico’ dhidi ya Real Madrid jijini Dallas, Marekani ukiwa mchezo wa pili kati ya mitatu ya Barcelona katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya.

Related Articles

Back to top button