Kwingineko

Napoli vs Barcelona: Ni kisasi UCL

KIVUMBI cha michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UCL) kinaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Italia na Ureno.

Miamba ya Hispania, Barcelona itakuwa mgeni wa Napoli kwenye uwanja wa Diego Armando Maradona uliopo jiji la Naples, Italia.

Mchezo huu ni wa kisasi, Napoli ikitaka kulipiza kisasi dhidi ya Barca kwani katika michezo ya mashindano yote ambayo timu hizo zimekutana kati ya mwaka 2011 na 2022 Barcelona imeshinda mara 5 zimetoka sare mara 2 na Napoli kushinda mara 1 tu.

Katika mchezo wa Ureno, wenyeji FC Porto itaikaribisha Arsenal kwenye uwanja wa Dragao uliopo jiji la Porto.

Matokeo ya mechi mbili za UCL zilizofanyika Februari 20, Inter imeshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Atletico Madrid mjini Milan wakati Borussia Dortmund imelazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya PSV Eindhoven.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button