Jikoni

“Mwanamke upishi babu!”

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo fleva nchini Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amewapa neno wasanii wenzake na mabinti wa Kitanzania kujifunza kupika kutokujuwa kupika ni aibu kwa mwanamke.

Shilole amesema anatarajia kuanzisha darasa la mapishi kwa wasanii wasiojua kupika ili waweze kujifunza.

“Darasa langu naamini litawapata wasanii wengi na vijana hasa mabinti sababu nawajua wasiojua kupika ni pamoja na wadogo zangu kama Linah na Nandy mara nyingi wanashinda Shishi food kujipatia chakula.”

“Nikiwa kama dada yao nawapa nafasi ya upendeleo kujifunza kupika mapishi tofauti na yeyote atakaye hitaji kujifunza karibuni Raha ya mwanamke ni jiko yaani mapishi sio kitu kingine hiyo Siri nawapa.”amesema Shilole

Back to top button