Africa

Muigizaji wa Tiktok akana kupelekwa Olimpiki na Serikali

NAIROBI, Kenya: NYOTA na muigizaji wa Tiktok Azziad Nasenya amekanusha uvumi kuwa yeye ni sehemu ya wajumbe wa Kenya wanaosafiri kwenda Paris, Ufaransa kwa Michezo ya Olimpiki ya 2024.

Wakenya wengi wameelezea hofu kuwa huenda Waziri wa Michezo akajumuisha makumi ya washangiliaji katika safari hiyo yote kwenye bajeti ya walipa kodi huku wengine wakienda mahakamani kushinikiza kufanya hivyo.

Kupitia mtandao wake wa Instagram unaofuatiliwa na watu zaidi ya milioni 2.3, nyota huyo mrembo amesema kwamba yeye hakuwa mmoja wa watu ambao Wizara ya Mambo ya Vijana ilikuwa ikipanga Kwenda nae Paris, nchini Ufaransa.

Aliandika: “Mimi si sehemu ya wajumbe wa Kenya kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024. Kuhusika kwangu na Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi wa Ubunifu na Michezo kulijikita zaidi. karibu na Kamati ya Kiufundi ya Ubunifu ya Baraza la Talanta Hela, inayoongozwa na Daniel Ndambuki.”

Nasenya aliendelea kusema kwamba safari yake ya mwisho ya kwenda Dubai, ambayo ilizua utata na taarifa potofu mtandaoni, ilifadhiliwa kikamilifu na waandaaji wa mpango wa #VisitDubai na si serikali ya Kenya na kufichua zaidi kwamba ilikuwa ni safari ya kutungwa.

“Ningependa pia kuweka wazi kwamba safari yangu ya Dubai na maeneo mengine imefadhiliwa na mimi, wateja au familia na si kama inavyoelezwa kwamba nimefadhiliwa na Serikali ya Kenya,” alieleza.

“Kulikuwa na madai kwamba nilisafiri kwenda Dubai kwa kutumia pesa zilizokusudiwa kukarabati uwanja. Wakati huo nilikuwa Dubai nikirekodi maudhui ya kampeni ya #VisitDubai, safari ambayo ilifadhiliwa kikamilifu na mteja. Risiti ziko kwenye mitandao yangu ya kijamii, ili watu wathibitishe badala ya kuamini uvumi.”

Nasenya, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa mwaka wa 2020 baada ya kushiriki katika shindano la ngoma #Utawezana, pia sauti yake ilisikika mno katika mazungumzo yanayoendelea ya kundi la Gen-Z.

Kauli ya Nasenya inajiri baada ya shinikizo kubwa la umma kutolewa kwa Waziri wa Michezo Ababu Namwamba kuweka hadharani orodha kamili ya watu wote wanaosafiri kwenda Paris kwa Michezo ya Olimpiki.

Related Articles

Back to top button