Bundesliga
Man City yakomaa na Musiala
MANCHESTER City wanaongoza kwenye harakati za kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Jamali Musiala.
Kwa mujibu wa mtandao wa Independent wa Uingereza, Liverpool, Barcelona na Paris St-Germain pia wanamuwinda Mjerumani huyo.
Musiala amekuwa na kiwango bora Bundasliga hadi sasa ameshafunga mabao 10 kwenye michezo 28 ya ligi hiyo, pia ametoa pasi za mabao sita.
Mkataba wa Musiala utaisha 2026, mpaka sasa ameonesha mwelekeo mdogo wa kupanua au kuboresha mkataba huo.
Sio Bayern wala Musiala aliyetoa tamko lolote kuhusu uwezekano wa kuendelea kukipiga Munich, huku baadhi ya vilabu vikijipa matumaini ya kumsana kiungo huyo.