Tetesi

Liverpool, Arsenal zamwania Zubimendi

TETESI za usajili zinasema Liverpool ipo tayari kushindana na Arsenal kumsajili kiungo mhispania Martin Zubimendi, 25, toka Real Sociedad. (Football Transfers)

AC Milan inafikiria kumteua kocha wa zamani wa Brighton na Chelsea,Graham Potter kuwa kocha wake mwisho wa msimu(Talksport)

Arsenal imekuwa ikimfuatilia winga wa Athletic Bilbao na Hispania, Nico Williams, 21.(Mirror)

Newcastle United ina nia kumsajili kiungo wa Ubelgiji na Everton, Amadou Onana, 22.(Football Insider)

Mshambuliaji wa Juventus, Dusan Vlahovic ni mlengwa mkuu wa usajili wa Chelsea wakati wa dirisha kubwa la uhamisho majira ya kiangazi. (Fichajes – Spain)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button