Nyumbani

Kocha wa zamani Simba afariki dunia

ALIYEKUWA kocha wa viungo wa Simba SC, Adel Zrane amefariki dunia leo nchini Rwanda.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo leo imetoa pole kwa familia na timu ya APR ya Rwanda na wadau wote.

Kocha huyo alijiunga na Simba msimu wa 2018 na kuondoka 2021 katika benchi la ufundi la timu hiyo.

“Zrane alikuwa mtu mkarimu sana, mcheshi na rafiki kwa wachezaji alipendwwa na kila mmoja,” imeeleza taarifa hiyo.

Related Articles

Back to top button