Jorginho aongeza Mwaka Arsenal

LONDON: KIUNGO wa Arsenal, Jorge Luiz Frello ‘Jorginho’ ameongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kundelea kuitumikia klabu hiyo.
Jorginho ,32, raia wa Italia alijiunga na Arsenal Januari 2023 akitokea Chelsea na amekuwa sehemu muhimu ya wakati huo akicheza zaidi ya mechi 50 katika mashindano yote.
Nyota huyo alianza soka lake akiwa na klabu ya Hellas Verona ya nchini Italia, ambapo aliingia katika kikosi cha vijana na kuchezea kikosi cha kwanza, na kucheza mechi 96 kwa jumla.
Jorginho kisha akasajiliwa na timu nyingine ya Serie A Napoli Januari 2014 na kukaa huko kwa misimu minne, akicheza mechi 160 na kushinda Coppa Italia na Supercoppa Italiana katika mwaka wake wa kwanza.
Jorginho alisajiliwa na Chelsea Julai 2018. Katika muda wa chini ya miaka mitano kusini-magharibi mwa London, alicheza mechi 213, akifunga mabao 29, na kusaidia mara nane, akishinda mataji manne makubwa.
Pia ameichezea Italia mechi 52 tangu aanze kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2016.
Mnamo 2021, Jorginho alishinda Champions League na UEFA Super Cup akiwa na Chelsea, na pia Euro 2020 akiwa na Italia. Hii ilimpelekea kutawazwa na tuzo ya mtu binafsi ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa UEFA.