Tetesi

JKT Tanzania: Malale Hamsin ‘out’ Ahmad Ally ‘in’

DAR ES SALAAM: BAADA ya Uongozi wa JKT Tanzania kutangaza kuvunja benchi la ufundi, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Ahmad Ally, anatajwa kwenda kukinoa kikosi hicho akichukuwa nafasi ya Hamsin Malale.

Imeelezwa kuwa Tanzania Prisons hawakutaka kuachana na Ahmad lakini kocha huyo aliamua kuachana na Tanzania Prisons baada ya kuwa na uhakika wa kupata dili la kwenda kukinoa kikosi cha JKT Tanzania kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

“Tanzania Prisons hawakutaka kuachana na Ahmad kwa sababu ya dili hilo ameamua kuondoka na sasa anaenda kukamilisha dili lake la JKT Tanzania, msimu ujao anatarajiwa kuwa sehemu la benchi la ufundi,” amesema mtoa habari huyo.

Spotileo lilimatafuta Katibu Mkuu wa JKT Tanzania, Speratus Lubinga amesema wameanza kuvunja benchi la ufundi lote ambalo lilikuwa chini ya Kocha Malale na kuwashukuru kwa utendaji wao wa kazi kwa kipindi chote cha msimu.

Amesema lengo la kuvunja benchi la ufundi kwa ajili ya kuboresha kikosi cha timu hiyo kwa kuanza benchi la ufundi na baada ya wataangalia masuala ya usajili wa wachezaji wapya kulingana na mahitaji ya timu.

“Tutafanya maboresho ya timu yetu, tumeanza na kuvunja benchi la ufundi na muda utakapofika tutaweka wazi atakayekuja kuchukuwa nafasi yake, pamoja na kufanya usajili mzuri kulingana na mahitaji yetu kwa msimu ujao,” amesema Katibu huyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button