Tetesi

Dortmund yashindwa kumsajili Sancho jumla

TETESI za usajili zimesema klabu ya Borussia Dortmund haiwezi kumsajili kwa mara nyingine kwa mkataba wa kudumu winga Jadon Sancho, 24, kutoka Manchester United. (Sky Sports), external

Everton inajiandaa kuwauza nyota wake kadhaa majira haya ya kiangazi wakiwemo golikipa wa England, Jordan Pickford, 30, na Beki Jarrad Branthwaite, 21, ambaye ni mlengwa wa usajili wa Manchester United. (Sun), external

Tottenham Hotspur inaweza kumsajili fowadi Ivan Toney, 28, kutoka Brentford majira haya ya kingazi kwa dili lenye thamani ya pauni mil 40. (Football Insider), external

Kiungo mhispania wa Real Sociedad, Martin Zubimendi, 25, hana nia kujiunga na Arsenal licha ya The Gunners kuonesha shauku kubwa kumsajili. (Sport – in Spanish)

Fowadi wa England Mason Greenwood, 22, anakaribia kujiunga na Juventus akitokea Manchester United. (Sun)

Arsenal ina shauku kumsajili fowadi wa Napoli forward Victor Osimhen, 25, baada ya Chelsea kushindwa kuendelea na majadiliano kumsajili nyota huyo wa Nigerian. (Gianluca di Marzio)

West Ham imefikia makubaliano binafsi na winga wa Palmeiras ya Brazil, Luis Guilherme, 18, ambaye atajiunga na timu hiyo kwa uhamisho wa pauni mil 25.6. (UOL – in Portuguese)

Galatasaray ina nia kumsajili kiungo wa Ujerumani na klabu ya Barcelona Ilkay Gundogan, 33, kuimarisha kikosi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.(90min)

Related Articles

Back to top button