Kwingineko

Demarai Gray atimkia Uarabuni

DEMARAI Gray ameikacha Everton ili kujiunga na Al-Ettifaq inayoshiriki Ligi ya Kulipwa Saudi Arabia.

Ada ya uhamisho haijawekwa wazi lakini ripoti zimesema winga huyo raia wa Jamaica mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Al Ettifaq kwa dili lenye thamani ya pauni milioni nane sawa na shilingi bilioni 24.5.

Grey alikemewa na kocha wa Everton Sean Dyche baada ya kuonekana kumkosoa kocha wake kupitia mitandao ya kijamii kufuatia mpango wa uhamisho wake kwenda Fulham kukwama.

Gray ameandika kwenye Instagram Septemba 7: “Ukweli ni kuwa nimejitolea vyote kwa ajili ya klabu hii ndani na nje ya uwanja. Nilikuwa tayari kucheza mpira kiwango chote kinachowezekana msimu huu lakini ilihisiwa kama vile haitatokea.”

Dyche amemjibu Gray kwa kusema kwamba hakuna uhamisho unaoruhusiwa bila klabu kuwa na uamuzi wa mwisho.

Gray amefunga mabao tisa katika michezo 67 Ligi Kuu England baada ya kuwasili Goodison Park mwaka 2021.

Al- Ettifaq inanolewa na nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard na hadi sasa imewasajili kiungo wa England Jordan Henderson, kiungo wa zamani wa Liverpool, Georginio Wijnaldum, beki wa Scotland, Jack Hendry na mshambuliaji wa zamani wa Lyon, Moussa Dembele.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button