Kikapu

Boston Celtics Mabingwa wapya NBA

Timu ya Boston Celtics imetwaa taji la Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani msimu wa 2023/2024 baada ya kuitandika timu ya Dallas Mavericks kwa vikapu 106-88 katika mchezo wa awamu ya tano.

Ubingwa huu ni rekodi kwa timu hiyo ikiwa ni mara ya 18 kufanya hivyo, mara nyingi zaidi kuliko timu nyingine yoyote ikifuatiwa na Los Angeles Lakers iliyobeba mara 17.

Ushindi huo ulichangiwa na viwango bora vya wachezaji kama Jayson Tatum aliyefunga vikapu 31,rebounds 8 na kutoa pasi 11 zilizozalisha vikapu. Jrue Holiday alimaliza mchezo akiwa na vikapu 15 pamoja na rebounds 11.

Jaylen Brown amechaguliwa kama Mchezaji Bora wa michezo ya Fainali (FINALS MVP) na katika mchezo huu alimaliza akiwa na vikapu 21.

Rekodi nyingine iliwekwa na kocha Joe Mazulla mwenye miaka 35 ambaye amekuwa kocha mwenye umri mdogo zaidi kutwaa ubingwa wa NBA tangu Bill Russel mnamo mwaka 1969.

Related Articles

Back to top button