Tetesi

Barca yamhitaji Lo Celso kwa mkopo

TETESI za usajili zinasema Barcelona inafikiria kumsajili kwa mkopo kiungo wa Tottenham na Argentina, Giovani Lo Celso, 27, Januari 2024.(90min)

Mazungumzo yanaendelea kuhusu klabu ya Eintracht Frankfurt kumsajili kwa mkopo kiungo wa Manchester United mdachi Donny van de Beek, 26.(Fabrizio Romano on X)

Arsenal imetuma ofa ya pauni milioni 17.2 pamoja na nyongeza kumsajili fowadi wa Santos na Brazil U20, Marcos Leonardo, 20.(Fichajes – in Spanish)

Manchester City inaweza ikatuma maombi kusajili kiungo na mshambuliaji katika dirisha dogo lijalo la uhamisho, Januari, 2024.(Football Insider)

Chelsea ina nia kumsajili fowadi wa Sweden anayekiwasha Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, 25.(Ekrem Konur on X)

Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu England vinavyomfuatilia winga wa Real Betis na Hispania U21, Assane Diao, 18.(TeamTalk)

Related Articles

Back to top button