Kwingineko

Antony kuanza mazoezi Man United

WINGA wa Manchester United kutoka Brazil Antony Matheus dos Santos maarufu ‘Antony’ ambaye anashutumiwa kwa unyanyasaji nyumbani atarejea kwenye mazoezi, klabu imesema.

Antony mwenye umri wa miaka 23 amezungumza na Polisi wa Greater Manchester Septemba 28 na hakuna vikwazo vilivyowekwa kwake kufuatia mahojiano hayo.

Vyanza vya habari vya United vimesema ametoa ushahidi wa kupinga vikali shutuma hizo.

Hajakamatwa au kufunguliwa mashitaka Brazil au Uingereza.

Katika taarifa United imesema: “Kama mwajiri wa Antony, Manchested United imeamua kwamba atarejea kwenye mazoezi Carrington na kupatikana kwa ajili ya kucheza huku uchunguzi wa polisi ukiendelea.”

Hata hivyo Antony hakutarajiwa kwenye mazoezi leo na hatakuwemo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kwenye uwanja Old Trafford kati ya Manchester United na Crystal Palace.

Hajacheza michezo minne tangu Man United ilipompatia likizo ya malipo kamili ili ashughulikie shutuma zilizotolewa na wanawake watatu tofauti akiwemo mpenzi wake wa zamani, Gabriela Cavallin.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button