Kwingineko
Anafunga tu huyu baba!

Goli la mkwaju wa penalti la Harry Kane lililofungwa dakika ya 18 ya mchezo wa nusu fainali ya Euro 2024 Kati ya Uholanzi na England, linamfanya mfungaji huyo wa England kuwa mfungaji bora wa muda wote wa hatua ya mtoano ya michuano hiyo akiwa na magoli sita.
Rekodi hiyo hapo awali ilishikiliwa na Mfaransa Antoine Griezmann aliyekuwa na magoli matano.
Ikumbukwe mshambuliaji huyo anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich alivunja rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa taifa lake la England katika mechi za kufuzu kwa Euro 2024 akifunga magoli 54 ndani ya mechi 90 akimpiku Wayne Rooney alikuwa anashikilia rekodi hiyo kwa magoli 50.